Array ( [0] => homepage [1] => Indundi Cinema [2] => Movies [3] => swahili )

 

Lokata Pierre maarufu kama Young Pdk Producer na Director wa Filamu ambae anaishi America mwenye uraia wa Burundi Baada ya kushuka nchini ya asili mwaka 2018 aliweza kuandaa Movie na akasimama mwenyewe kama Cameraman ila ameshirikisha wa cameraman wengine kama Hugues Banana na John Elart, ili kuleta ujuzi tofauti na akaweza kufanikisha project hiyo maana ameshirikisha wasanii wakubwa wenye uwezo wa uchezaji kama Tambwe Remy, Harerimana Hamu, Itangishaka Julien na wengineo.

Basi katika maojiano na indundi, Pdk ameongea nakusema:

“Mimi kwanza naamini nini nilicho kuja kukifanya Burundi pia nimeandaa project hii takribani miaka 2 na baadae nilivyoshuka Burundi nikakutana na waigizaji wazuri na wenye moyo wakupenda kazi kwa hio kazi imekuwa nzuri sana pia ni filamu iliobeba story nzuri sana yenye uzuni, Mateso, Mapenzi na Furaha kwa hio mashabiki wa Buja Movie wategemee kitu kizuri japo naandaa mazingira ya kuzinduwa”.
Alisema Young Pdk

Kiupande wa maendeleo nchini Burundi tunaona kwa kweli imepiga hatuwa baada ya John Key kutoka Australia nakuja kuzinduwa filamu yake apa sasa ni zamu ya Pdk.

Indundi inawatakia maendeleo mema pia nakuwaambia wadhamini wanao itaji kusapoti kazi wajiitokeze kwa wingi.